Baada ya kuonekana kuwa ukiukwaji wa maadili Tanzania ni miongoni mwa
majanga ya kitaifa yanayotakiwa kupigiwa filimbi ya hatari mapema kuokoa
kizazi hiki, serikali imenyoosha mkono wake kwa baadhi ya wasanii na
waburudishaji walioonekana kuwa sehemu ya tatizo hili.
Akijibu swali lilioulizwa jana bungeni na mbunge Catheline Magige,
Naibu Waziri wa habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Juma Nkamia
alifafanua hatua zilizochukuliwa na serikali kupitia wizara yake
kuhakikisha wanakomesha mapema vitendo hivyo.
Nkamia alieleza kuwa serikali ilishafanya vikao na wamiliki wa kumbi
mbalimbali za starehe, wamiliki wa bendi, maafisa utamaduni na wakuu wa
jeshi la polisi.
Baada ya vikao hivyo, serikali ilizuia kutoa kibali kwa vikundi vya
Kangamoko kutokana na jinsi vikundi hivyo vinavyotumbuiza kwa mitindo
inayokiuka maadili ya Tannzania na pia wametoa onyo kwa wasanii wa
filamu na muziki wa kizazi kipya.
“Mfano wasanii waliopewa onyo ni Nay wa Mitego, Shilole na Anti
Ezekiel. Na kwa upande wa kumbi ni Mamas &Papas.” Nkamia ameeleza.
Ameongeza kuwa serikali imeunda kamati ya kitaifa ya kuzuia vitendo
vya ukatili, unyanyasaji wa watu wenye ulemavu wa ngozi na watoto, na
vitendo vyote vya udhalilishaji wa wanawake.
Wiki kadhaa zilizopita, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudencia Kabaka
alimsifia Nikki wa Pili kupitia wimbo wake wa Staki Kazi kama mfano wa
kuigwa kwa vijana wanaotegemea kuajiriwa.
Wednesday, 4 June 2014
New
BAADA YA SHILOLE NIKI WA PILI KUSIFIWA NEY WA MITEGO WATAJWA TENA KIVINGUNGINE CLICK KUSOMA
About Cow Boy Bishoo Tz
SoraTemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of SoraTemplates is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)




No comments:
Post a Comment