HUU NI MCHONGO ANAO USUKA RAPPER MABESTE SOMA NDANI............. - COW BOY BISHOO

Breaking

Thursday, 5 June 2014

HUU NI MCHONGO ANAO USUKA RAPPER MABESTE SOMA NDANI.............

 Mabeste, jina la rapper aliyekuwa akifanya kazi katika label ya B’Hitz ni moja kati ya wasanii ambao CEO wa BHitz Hermy B anaowamiss.
Siku moja baada ya Hermy kuzungumza kuwa ameimiss timu ya wasanii wa BHitz iliyokuwa ikiundwa na Mabeste, Vannesa, Gosby, Deddy, MRap na DJ Choka, Mabeste amepiga story na E News ya East Africa Radio kuhusu kile anachokifanya.
Amesema hadi sasa bado hajapata label ya kufanyia kazi na anaendelea kusaka mchongo wa label yenye vigezo anavyotaka.
“Unajua nilivyokuwa pale, sio kwamba hakuna mapungufu yanayotokea. unajua unapofanya kazi na group ama sio peke yako, obvious unapotoka na ukataka kuanzisha chako lazima hapo katikati utayumba. Kwa sababu kuna baadhi ya vitu vilikuwa vinafanywa na watu.
“Na record label… yeah, nikipata record label ambayo iko poa ambayo naoka kama ina muziki mzuri jinsi navyotaka mimi Mabeste tutafanya. Ila bado nafanya mimi mwenyewe. Nikipata record labe ntafanya pia.”

No comments:

Post a Comment