Hii
imetokea Mkoani Arusha leo hii, Chatu mkubwa akiwa amefungwa kitambaa
cheupe chenye maandishi ya kiarabu amekutwa kwenye nyumba ya mkazi mmoja
wa Eneo la Sakina.
Majirani
walipoanza kumvizia ili waweze kumuua walipata taarifa ya simu kutoka
kwa Mwenye nyumba hiyo ambae ni tajiri mmoja wa huko Arusha akidai kuwa
wasimuue huyo mtoto wake, lakini majirani hao hawakufata vile ambavyo
huyo Mama alidai na hatimae walifanikiwa kumuua na kumkata kata vipande.
Baadhi
ya watu wamehusisha kitendo hicho na imani ya kishirikina (Uchawi)
hivyo kupelekea watu kuamini kuwa hata utajiri wake umetokana na mambo
hayo.
No comments:
Post a Comment