USHER ALIVYO MTETEA JUSTINI BEBER KUHUSU UBAGUZI WA RANGI SOMA - COW BOY BISHOO

Breaking

Monday, 9 June 2014

USHER ALIVYO MTETEA JUSTINI BEBER KUHUSU UBAGUZI WA RANGI SOMA

 Kwa muda wa wiki mbili zilizopita mwimbaji JustinBieber aliwekwa kwenye kaa la moto la mashambulizi ya maoni ya watu mbalimbali waliomkosoa baada ya kuvuja kwa video vinazomuonesha akifanya utani wa ubaguzi wa rangi.
Usher na Bieber
Justin aliomba radhi baada ya video ya kwanza kutoka lakini kabla ombi lake halijafika mbali iliachiwa video nyingine ya pili inayomuonesha akifanya vilevile kwa kubadili maneno ya wimbo wake na kutumia N-Word. Video zote alirekodi akiwa mtoto mwenye umri wa mika 15.
Mzigo umekuwa mzito kwa Justin Bieber kutokana na jinsi dunia inavyochukulia kwa umakini masuala ya kibaguzi.
Usher Raymond ambaye alimgundua msanii huyo kupitia YouTube, ameamua kumsaidia na kuandika ujumbe kwenye Instagram kumtetea kwa kuwa anajua alikuwa mtoto mdogo.
“Mimi ni mtu ambaye nasapoti ukuaji na naelewa bila hukumu. Ukuaji huo unakuja kama matokeo ya maumivu na bidii endelevu. Kama nilivyokuwa nikiangalia magumu anayopitia Justin Bieber kama kijana mdogo. Naweza kuwaambia kuwa daima hakuchagua njia ya uwezekano wake kuwa mkubwa zaidi. Lakini bila utata wowote sio mbaguzi wa rangi.
Allivyokuwa miaka 5 iliyopita alikuwa ni mtoto asiye na uelewa na busara ambaye hakuelewa nguvu hasi na kutojali utu vinavyotokana na kucheza na mzaha wa kibaguzi. Jinsi alivyo sasa ni kijana mdogo ambaye banakabiliwa na fursa za ku
wa bora zaidi, mfano kwa mailioni ya watoto wanaomfuata ili wasifanye kosa hilo.”

No comments:

Post a Comment