Kwa mujibu wa mtandao unaomilikiwa na 50 Cent, kundi hilo liko studio
hivi sasa likipika albam yao mpya ambayo inatarajiwa kutoka November
mwaka huu.Wasanii waliokuwa wakiunda kundi hilo na baadae kugombana wameelezea jinsi walivyofikia uamuzi wa kuyamaliza na kuirudisha Gorilla Unit.
“Tulikaa mezani, na ikafanyika… ni hivyo. Iko poa. Sisi ni ndugu. Hakuna kitu kinachotushinda kukimaliza. Ndugu hugombana muda wote. Tumeachia ngoma mpya jana. Tunafanya kazi” Amesema Tony Yayo.
Nae Young Buck aliliambia XXL kuwa wako studio na wanaendelea kuandaa vitu watu wavisubirie. “Work in progress. We just put out the new freestyle today. Check it out.” Aliongeza Banks.

No comments:
Post a Comment