Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini Tanzania
leo imepokea taarifa kutoka ubalozi wa Libya nchini ikieleza kuwa
aliyekuwa Kaimu Balozi wa Libya Bw. Ismail Nwairat, amefariki dunia jana
kwa kujipiga risasi.
Taarifa hiyo ya ubalozi imeeleza kuwa kifo hicho kimetokea majira ya
saa saba mchana ofisini kwa Kaimu Balozi huyo katika jengo la Ubalozi wa
Libya ambapo imeelezwa kuwa marehemu alijifungia ofisini na
kujifyatulia risasi kifuani upande wa kushoto.
Maafisa ubalozi walivunja mlango waliposikia mlio wa bunduki na
kumkuta Kaimu Balozi Nwairat ameanguka chini na kuamua kumkimkimbiza
hospitali ya AMI iliyopo Oysterbay ambako alitangazwa kuwa
amekwishafariki dunia, kifo ambacho kimethbitishwa pia na jeshi la
polisi kanda maalum ya Dar es Salaam.
Mwili wa marehemu Nwairat umehamishiwa hospitali ya taifa Muhimbili
na kwa sasa ubalozi unafanya maandalizi ya kusafirisha mwili wake kwenda
nchini Libya kwa mazishi.
Wednesday, 2 July 2014
New
Jua Taarifa Ya Kaimu Balozi Wa Ribya ,Aliye Jiua Kwa Kujipiga Lisasi Taarifa Ziko hapa clik Picha Kujua
About Cow Boy Bishoo Tz
SoraTemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of SoraTemplates is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment