JESHI
la polisi mkoani hapa limewaua majambazi watatu waliokuwa wamepanga
njama ya kwenda kupora mamilioni ya fedha zilizokuwa zinapelekwa benki
na kampuni ya Arusha Islamic Centre inayohusika na utengenezaji na
uuzaji wa vigae iliyopo eneo la Esso mjini hapa.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa polisi
mkoani hapa, Liberatus Sabas alisema kuwa,majambazi hao watatu waliuawa
jana tarehe 3 eneo la TBL -Njiro wakiwa kwenye harakati za kwenda
kupora fedha hizo.
Alisema kuwa, majambazi hao walikuwa mahali wanapanga njama majira ya
saa 4;20 asubuhi wakisubiria kuteka gari lililokuwa limebeba fedha
zilizokuwa zinapelekwa benki zaidi ya milioni 100 huku wakiwa na gari
aina ya Toyota Corola yenye namba za usajili T 762 CWE.
Alisema kuwa, raia wema walitoa taarifa kuhusiana na tukio hilo ndipo
polisi walifika eneo ambalo majambazi hao walikuwa wamejificha katika
eneo la unga ltd relini ambapo majambazi hao walishtuka na kuanza
kuirishia gari hiyo ya polisi risasi.
Ambapo majibizano
yalianza kati ya majambazi hao na polisi huku wakirushiana risasi hadi
eneo la TBL njiro ndipo majambazi walipofika eneo hilo waliamua
kutelekeza gari na kushuka chini na kumimina risasi kwa askari polisi
hao.
Kamanda Sabas alisema
kuwa,hatimaye polisi waliweza kuwauawa majambazi hao na kufanikiwa
kuchukua silaha yao aina ya shortgun yenye namba A 947514 M aina ya
Pumpaction ikiwa na risasi 3 .
Kamanda alisema kuwa,
bado majina ya majambazi hayo hayajafahamika ambapo wanakadiriwa kuwa na
umri kati ya miaka 25 hadi 30 na miili yao imehifadhiwa katika
hospitali ya mkoa ya mount Meru.
Aidha
Kamanda aliwashukuru wananchi kwa juhudi kubwa sana walizoonyesha na
ushirikiano hadi kukamatwa kwa majambazi hayo na kuwataka kuendelea
kuongeza juhudi hizo zaidi.
No comments:
Post a Comment