
Siku mbili zilizopita kumekuwa na taarifa
mitaani kuwa mwimbaji ambaye pia ni producer wa Sharobaro Records, Bob
Junior alifanyiwa fujo na mwanaume mmoja anaedaiwa kuwa mume wa msichana
aliyekuwa anafanya naye video.
Taarifa hizo zilieleza kuwa tukio hilo
lilifanyika maeneo ya Mlimani City wakati Bob Junior alipokuwa akishuti
vipande vya wimbo wake wa ‘Bolingo’ huku msichana huyo akijiachia mbele
ya lens.
Ghafla mumewe akatokea na kuzua tafrani,
video ya wimbo ikageuka kuwa ya ndondi na mwisho wa siku mwimbaji huyo
alilazimika kukimbia kupisha shari.
Tovuti ya Times Fm imeongea na Bob Junior
kuhusu tetesi hizo ambapo yeye amekiri kutokea kwa fujo hiyo lakini
amekanusha kuhusu suala la kufanya video na msichana huyo ingawa alikuwa
na directors wake na vifaa.
“Hapana, naona watu wanakuwa kama wambea.
Mimi nilikuwa nimekaa pale Mlimani City tunapiga story niko na mwanamke
wangu. Rafiki yangu mwingine alikuwa kaka na mwanamke mwingine, sasa
sijui kama ni mke wa mtu au nini, ndio ikatokea vurugu lakini huyo
mwanamke aliyefanyiwa vurugu mimi simfahamu.” Ameeleza Bob Junior.
“Tulikuwa tumekaa tu tunaenjoy tunapiga
story, tunakula…mimi sijui kama ni mwanamke wake au ni mke wake.
Amemfanyia vurugu, amemvuta nywele. Wamezinguana kidogo lakini sifahamu
kama ni mke wake au ni mchumba wake ila najua ni mtu ambaye ana uhusiano
nae.” Ameongeza.
Akizungumzia kuhusu taarifa kuwa alitoka
nduki na kumuacha rafiki yake akifanyiwa fujo, Bob ameeleza kuwa
aliondoka kupisha shari na sio kukimbia kama ilivyotafsiriwa.
“Hapana siwezi kukimbia siwezi kukimbia.
Tanzania ni nchi yenye amani kwa nini nikimbie kuna vita gani jamani
hapo. Mimi nilichukua vitu vyangu na vijana wangu na team Sharobaro
wangu, nikaondoka taratibu nikachukua gari langu nikaondoka. Unapoona
mtafaruku hupaswi kukaa kuendelea kuangalia jambo.

No comments:
Post a Comment