Producer Monagangstar aliyeripotiwa kuwa ndiye msimamizi wa kazi za
Young Killer amesema kuna mambo tofauti anafanya rapper Young Killer
yanayoashiria utovu wa nidhamu na kinyume na mkataba. Monagangstar
anasema Kuna kitu kipo tofauti na tulivyoanza kufanya kazi Na Young
Killer…..
“Young Killer amebadilika,amekuwa maarufu na ameshikwa masikio na
watu, Bado nina mkataba na Young Killer mpaka December 2014 ila
anaukiuka mkataba huu kwa kwenda kufanya kazi studio zingine na sasa
hata Classic Sounds hafiki, Classic Sounds haim’bani msanii ila akitaka
kufanya kazi nje ya studio hii ni lazima tubaki kama Executive Producer
wa kazi hio ilituhakikishe kiwango cha kazi ni bora, Young Killer
amefanya kazi nje ya studio bila taarifa wakati mkataba wa Classic
Sounds hauruhusu hicho kitu” Alisema Monaganster
Hii sio mara ya kwanza kusikia taarifa za kutofautiana kwa Young Killer
na Monagangstar, kama wiki chache nyuma palikuwa na uvumi kuwa wawili
hawa hawafanyi kazi pamoja na Young Killer alivunja mkataba. Young
Killer amefanya kazi yake mpya studio za Combination Sounds kwa Man
Water, Kazi mpya inaitwa Umebadilika
Saturday, 2 August 2014
New
Producer Monagangstar Alalamika Kuhusu Tabia Ya Young Killer
About Cow Boy Bishoo Tz
SoraTemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of SoraTemplates is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment