kariakoo jinsi maduka yalivyo fungwa |
maduka kama hivi unavyo ona |
wauzaji wamesusa |
kujua mengi zaidi ndugu tembela ukurasa wangu wa pge ya cowboybishootz.blogpost.com |
Dar es Salaam. Wafanyabiashara wachache waliofungua maduka eneo
la Kariakoo jijini hapa, wamewataka wenzao wanaoendelea na mgomo
kukubali amri ya Serikali ya kutumia mashine za risiti za kielektroniki,
EFD, kwa kuwa zina manufaa kwa nchi.
Wakizungumza na Mwananchi kwa nyakati tofauti
walisema hawaoni haja ya kuendelea kupingana na agizo hilo, ilhal
ulipaji kodi unachangia katika kuboresha huduma za kijamii na maendeleo
ya nchi.
Juma Beku anayefanya biashara ya kuuza nguo za
mitumba alisema aliamua kuanza kutumia mashine hizo mapema, hivyo
hajaathirika kibiashara kutokana na mgomo huo.
Alisema wafanyabiashara wengi wameingia kwenye
mgomo kwa kufuata mkumbo pasipo kufanya tathimini ya kina juu ya athari
zake, kwani licha ya kutofanya biashara kwa kipindi hicho, itakapofika
mwisho wa mwezi mwenye jengo atahitaji kodi yake.
Mohamed Kasanga alisema waliofunga maduka
hawatambui kile wanachokihitaji, kwani hakuna nchi iliyoendelea duniani
ambayo haibani wananchi wake katika ulipaji kodi.
Aliwataka wafanyabishara hao kuacha kufuata mkumbo kwani kila
mtu alianzisha biashara akiwa peke yake na hata kama itatokea akapata
hasara, yeye ndiye atakuwa mwathirika .
“Ninachoweza kuwashauri wenzangu ni kukubali
kuzitumia mashine hizi kwa sababu kama ni hasara hata hili jambo la
kufunga maduka kwa siku nne mfululizo sasa ni la hasara zaidi,” alisema.
Aliongeza kusema: “Hakuna mtu aliyewalazimisha
kufunga maduka. TRA walisema watapita kukagua wanaotumia mashine, sasa
wao wanafunga wanaogopa nini? Wanachotakiwa kufanya ni kufuata sheria.”
Salum Hussein alisema anaunga mkono hatua ya TRA
kutaka wafanyabiashara kutumia mashine hizo na kwamba wale wanaopinga,
ndiyo waliokuwa wanakwepa kulipa kodi halali.
Baadhi ya waliofunga maduka kupinga matumizi ya
mashine hizo walikataa kuongea kwa madai kuwa vyombo vya habari vimekuwa
vikiwanukuu tofauti na wanavyoeleza.
Jana saa 4:00 asubuhi maduka mengi katika eneo la Kariakoo yalikuwa yamefungwa na kusababisha wateja kuhangaika kutafuta huduma.
No comments:
Post a Comment