‘Aliniambia by the way nilikua nataka kama unaendelea kuvuta, naona
mambo ya kuvutavuta umeachana nayo, tunakaa karibia muda wote
tunazunguka wote hata kunywa nimesimama kwa hiyo sasa hivi sio tena muda
wa kujielezea oooh navuta, oooh sivuti oooh nakunywa…. naendelea na
maisha yangu kama kawaida’
Kuhusu kukamatwa Aiport na dawa za kulevya Benz amesema ‘Sikuwaambia Polisi kwamba natumia dawa walizonikamata nazo, niliwaambia dawa nilizokua nazo lazima nilikua nimechanganya kipindi nilikua nazitumia nilikua nafichaficha kwenye nguo zangu, enzi zile nilikua naficha dawa kwa kuziweka hivyo nikiwa sitaki mtu ajue’
‘Shetta aliponipigia simu ya fasta ili tusafiri kutoka Dar es salaam kwa
ndege mpaka Mbeya nikalichukua tu shati na kulivaa na jeans na
nilivyofika Airport nikawa namtania tu Shetta namwambia mdogo wangu
nimebeba mambo kibao, mabegi yamejaa yote ila sina viatu wala nguo,
imagine nafika pale nasachiwa nakutwa na dawa kwenye mfuko wa shati
kushoto… sio kama nimeficha au nini’
‘Sio kitu nilikua nimepanga, sio kitu nilikua nimeplan…. mi mwenyewe
nimejisachi nikakutwa nayo, sijakamatwa…… mimi nimezitoa…. natoa hivi
nakutana na vidude kama kadhaa naviona tu mkononi hapa, jamaa akaviona
akaniambia hii nini? nikamwambia hii dawa lakini sijui imekuaje na mimi
pale kidogo kibinadamu akili ilikua imeniruka kugundua ile ni dawa na
nimeitoa mwenyewe’
‘Kama nilipigwa na butwaa hivi nikajaribu kuomba jamaa nikawaambia bwana
sorry kuna time nilikua natumia hizi vitu nikaachana nazo, so kama
mnaweza kunielewa mkanisamehe wakasema hakuna….. wakasachi kila begi na
hawakukuta kitu kingine’ – Chidi Benz
No comments:
Post a Comment