|
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
akizungumza na waandishi wa habari wa Zanzibar kwenye ofisi ndogo za
mashirika ya Umoja wa Mataifa visiwani Zanzibar kuhusiana na mafanikio
ya mradi wa kusaidia maendeleo nchini Tanzania (UNDAP) ulioanza mwaka
2011 na sasa ukiwa ukingoni. Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)
Tanzania, Zulmira Rodrigues na kushoto ni Mtaalam wa Mahusiano na
Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu.
Na Mwandishi wetu, Zanzibar
Zaidi ya watoto 3000 waliokuwa
wakikabiliwa na utapiamlo nchini Zanzibar sasa wapo katika hali nzuri
baada ya Umoja wa Mataifa (UN)kwa kushirikiana na wadau wengine
kufanikisha programu ya kusaidia kukabili utapiamlo mkali kwa watoto
hao.
kauli hiyo imetolewa katika mkutano
wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na waandishi wa habari uliofanyika hivi
karibuni ambapo UN ilielezea mafanikio ya mradi wa kusaidia maendeleo
nchini Tanzania (UNDAP) ulioanza mwaka 2011 na sasa ukiwa ukingoni.
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja
wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa
(UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez alisema kwamba Umoja huo ukiadhimisha
miaka 69 ya uwepo wake imefurahishwa na maendeleo yaliyopatikana katika
maeneo ambayo ilikuwa imejikita kusaidia kukabili umaskini,kuhakikisha
utawala bora na kusaidia jamii.
Alisema pamoja na kuendeleza na
juhudi za kukabiliana na utapiamlo katika visiwa vya Pemba pia Umoja huo
umefurahishwa na hatua zilizofikia katika kukabiliana na vifo vya mama
na mtoto na kusema ni wajibu kuhakikisha watoto hawana matatizo ya
utapiamlo kwani wao ndio msingi wa taifa la sasa na lijalo.
Alisema hata hivyo upo umuhimu wa
kuendelea na washirika wengine wa maendeleo kuona kwamba tatizo la
utapiamlo la visiwa vya Pemba kwa watoto linamalizwa.
|
Mwandishi wa habari wa TBC,
Kulthum Ally, akiuliza swali kuhusiana namna Umoja wa Mataifa
unavyoweza kuwasaidia Wanawake wa Zanzibar kupata nafasi za uongozi
sawa na wanaume.
|
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)
Tanzania, Zulmira Rodrigues akielezea kufurahishwa kwake na Serikali
Tanzania kwa kupigia hatua katika kutoa ajira nyingi kwa walimu kwenye
mkutano huo. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa
na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini,
Alvaro Rodriguez.
Alisema pamoja na mafanikio hayo
Umoja wa Mataifa unaendelea na ujenzi wa uwezo kwa baraza la
wawakilishi ili kuhakikisha kwamba baraza hilo linawezesha kuwepo kwa
sheria nzuri na bora na zinazotekelezeka ambazo hazikwazi kukua kwa
demokrasia na ustawi wa jamii.
Aidha alisema kwa kuzingatia kwamba
mwaka huu mwishoni kuna uchaguzi wa serikali za mitaa na pia uchaguzi
mkuu mwakani pamoja na kura ya maoni ya katiba, Umoja huo unaendelea
kufanyakazi na Tume ya uchaguzi ya Zanzibar kwa kuiwezesha kitaalamu
kuweza kufikisha elimu ya uraia kwa wananchi.
Aidha katika masuala ya utawala bora
Umoja wa Mataifa unashirikiana na taasisi za sheria kwa ajili ya
kufanya mabadiliko katika mfumo wa sheria za watoto ili kuwepo na
usalama mkubwa kwa watoto hasa kutokana na utamaduni uliopo visiwani kwa
sasa.
Aidha alisema kwamba yamepatikana
mafanikio makubwa katika sekta ya tiba na kuzuia maambukizi ya Ukimwi na
kuondokana na unyanyapaa.
|
|
Mwandishi wa gazeti la Mwananchi Zanzibar, Talib Ussi akiuliza swali kwenye mkutano huo.
Aliwahimiza waandishi wa habari kuwa
daraja la kuelezea mafanikio na pia changamoto zinazotokana na program
za Umoja wa mataifa zilizolenga kusaidia maendeleo ya wananchi wa
Zanzibar.
Alisema matokeo ya program ya
kusaidia maendeleo ya Tanzania (UNDAP) ndiyo yatakayotumika kutengeneza
UNDAP 2 ambayo inatarajiwa kuanza katikati ya mwaka 2016.
Katika mkutano huo ambapo waandishi
walipata nafasi kubwa ya kuuliza masuala yanayohusu shughuli za Umoja wa
Mataifa Zanzibar, Bara na duniani kwa ujumla Alvaro alizungumzia pia
umuhimu wa Umoja wa Mataifa katika dunia inayobadilika.
Alisema pamoja na madhumuni ya
kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa, baada ya vita kuu ya dunia ya pili
mwaka 1945 ya usalama na kujenga uchumi baada ya kuharibiwa na vita yapo
palepale, mabadiliko katika utendaji kwa lengo hilo hilo la usalama na
maendeleo ni dhahiri.
Alisema mathalani malengo ya
millennia (MDGs) ambayo yalisanifiwa kwa lengo la kuleta maendeleo
duniani katika demokrasia, utawala bora na ustawi wa jamii, bado
yanatakiwa kuimarishwa kupitia mpango mpya wa maendeleo SDGs wenye lengo
la kutokomeza umaskini uliotopea duniani ifikapo mwaka 2030.
|
Afisa Habari wa kituo cha habari
cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia Nkhoma Ledama akifafanua jambo
kwenye mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na mafanikio ya mradi wa
kusaidia maendeleo nchini Tanzania (UNDAP) ulioanza mwaka 2011 na sasa
ukiwa ukingoni.
Alisema ni matumaini yake kwamba
Tanzania itaendelea kushirikiana na UN katika kuhakikisha kwamba
mafanikio katika MDGs yanaendelezwa na pia kukamilisha yale ambayo
hayakufikiwa kwa lengo la kutokomeza umaskini uliotopea ifikapo mwaka
2030.
Alisema mafanikio ya UNDAP kwenye
utawala bora, ustawi wa jamii na uondoaji umaskini na ukuaji wa uchumi
nchini Tanzania, ni matokeo ya ushirikiano kati yake ya mamlaka
mbalimbali nchini Tanzania na kwamba UN itaendelea kushirikiana na
mamlaka hizo kuhakikisha maendeleo ya kuwezesha amani na usalama na
ukuaji wa uchumi yanapatikana.
Naye Afisa Habari wa Kituo cha
Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia Nkhoma Ledama amesema lengo
la kukutana na waandishi wa habari wa Zanzibar lilikuwa kuangalia
mafanikio na namna ambavyo program za Umoja wa Mataifa katika visiwa vya
Zanzibar zinafanyakazi.
Alisema kwamba shughuli za Umoja wa
Mataifa visiwani humo zinaweza tu kujulikana kwa wananchi kwa kupitia
waandishi wa habari ambao wanakuwa wanajua Umoja huo unafanya nini na
wapi.
|
Mratibu Mkazi wa mashirika ya
Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (waliokaa katikati), Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues (kulia) pamoja na Meneja
wa Baraza la Habari Zanzibar, Suleiman Omar (kushoto) katika picha ya
pamoja na waandishi wa habari wa Zanzibar.
|
Mkutano kati ya Mashirika ya Umoja wa Mataifa na waandishi wa habari wa Zanzibar ukiendelea COW BISHOO TZ NDIO CHOMBO CHAKO CHA HABARI NA NYIMBO MPYA BASI TUWE PAMOJA HUKU PIA>>>>
FACEBOOK>>>>>
TWITTER>>>>>
INSTAGRAM
No comments:
Post a Comment