Rapper mchanga, Young Tuso amemchana Nikki Mbishi aka Dr Unju, kwa kudai
kuwa msanii huyo ameshindwa kuhimili kasi ya rappers wapya na ndio
maana ametangaza kuacha kufanya muziki.
Tuso amemchana rapper huyo kupitia 255 ya XXL ndani ya Clouds FM,
Jumatatu hii. Pamoja na kumchana, Tuso amekiri kuwa hip hop bado
inamuhitaji Nikki.
“Hizi habari kwanza zimenisitua lakini naona pengine muziki wa Hip Hop
ulikuwa unamhitaji bado,” amesema Tuso. “Sijajua kwanini ameamua kuacha
muziki, sijajua kwa kweli. Yeye kama yeye ni msanii mkali ambaye
anajiamini, hakutakiwa kusema hivyo. Hivyo ni kusanda tu kwenye huu
muziki,” ameongeza.
“Unajua naweza nikasema ameacha kwenye huu muziki akiwa anazungumzia
sababu fulani kumbe inawezekana ni kusanda tu, kwamba Young mcees
wanakuja vizuri si wadogo, wanaendelea kuchachafya. Labda anaona siku
zinaenda halafu watu wanazidi tu kufanya mangoma, kwahiyo namhesabu kama
MC aliyesanda. Kwanini aache kama yeye ni msanii mkali kabisa wa Hip
Hop?, amehoji.
Tuso hakusita pia kufafanua maana ya ‘kusanda’.
“Kusanda ni kuchemsha kwenye jambo fulani, kushindwa, kwahiyo mimi
nikisikia yeye ameacha muziki naona amechemsha kwenye rap game.”
No comments:
Post a Comment