Jinsi Bi Rebeka alivyopigwa shoka kichwani hadi ubongo kutoka nje
Kwa mujibu wa majirani,
tukio hilo limetokea leo majira ya saa tatu asubuhi katika Mtaa wa
Nyahanga, wilayani humo, ambapo Marehemu Rebeka alienda nyumbani kwa
mtoto wake Bundala Sengasenga alikokuwa ameitwa na mke wa Bundala
kusaidia kuanika Dengu.
Katika maelezo yake
Magreth amesema Mama mkwe wake Marehemu Rebeka alifikia sebuleni, na
kwamba wakati yeye yuko nje, alimwona mtu ambaye hakuweza kumfahamu
akitoka sebuleni hapo na kukimbia ndipo alipoangalia na kumkuta Rebeka
ameuawa.
Taarifa za awali
zimedai, kabla ya tukio Magreth ambaye kwa sasa anashikiliwa na jeshi la
polisi mjini Kahama kwa mahojiano alienda nyumba ya jirani kuazima
Shoka, ambalo baadaye limekutwa kwenye shimo la maji taka nyumbani
hapo.
Mwili wa Marehemu Bi Rebeka ukiondolewa eneo la tukio kupelekwa Mochwari
Shoka hilo limepatikana
baada ya mbinu za kiupelelezi za Jeshi la Polisi kuagiza gari la maji
taka kuyavuta maji hayo baada ya majirani kudai hawajaona mtu
aliyekimbia na shoka muda huo katika mwelekeo ambao Magreth ameelekeza.
TOA MAONI YAKO MTU WANGU APO CHINI

No comments:
Post a Comment