 |
Add caption mkono nyumbani kwake wakati akila daku.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Sheikh Sudi amejeruhiwa sehemu mbalimbali
ikiwemo miguu yake yote miwili na sehemu za mapajani pamoja na Kifuani
na kupoteza baadhi ya vidole vya miguu yote miwili.
Akiwa kwenye hospitali ya mkoa Mount Meru, Sudi amesema ‘nilijikuta
tu nimeumia baada ya kutupwa bomu nyumbani kwangu na kuumia kwenye
miguu’
Muhaji Kifea (38) mkaazi wa Dar es salaam ambae alikua na Sheikh
wakati huo amesema ‘jana nilikua nimetokea Nairobi hivyo akawa
amenitengea chakula nikawa napata daku pale na wakati huohuo ndio bomu
likanilipukia na ilikua kama saa tano usiku hivi, walilirusha kupitia
dirishani na tayari walikua na vitisho juu yake, hata kwenye kutupa bomu
walitaka kumdhuru yeye sio mimi’
Hii taarifa imekuja wakati Mufti Issa Bin Shaaban Simba akiwa ametoa
tamko juu ya mgogoro wa muda mrefu wa uongozi kwenye msikiti mkuu wa
Ijumaa wa mkoa wa Arusha na msikiti mdogo na kuweka wazi viongozi
wanaostahili kuiongoza misikiti hiyo kisheria. |

Tamko amelitoa mbele ya baadhi ya Waumini na Viongozi wa kamati ya
ulinzi na usalama ya mkoa wa Arusha Sheikh na kusema viongozi wapya
waliopewa jukumu la kuongoza misikiti hiyo ambao waliondolewa na kikundi
cha Waumini, wako kwa mujibu wa sheria na ndio wanaotambulika na sio
vinginevyo.
Hata hivyo baada ya Sheikh Mkuu kutoa tamko hilo viongozi
walioondolewa madarakani wamesema hawatambui tamko la sheikh mkuu Mufti
Issa Shaaban kwani limetolewa wakati tayari kesi iko Mahakamani.
Sheik Simba alisema msikiti mkuu wa Ijumaa utaongozwa na Sheikh wa
mkoa Shaban Bin Jumaa Abdallah na kaimu katibu wa mkoa Ustadh Abdallah
Masoud na mwenyekiti wa halmashauri Ustadh Mohamed Juma Marawi na
msikiti wa Masjid Quba utaongozwa na Sheikh Hassan Waziri ambae ni imamu
na Abubakar Sharif huku mweka hazina akiwa ni Chohan Jumbe. MAONI YAKO
No comments:
Post a Comment