Kampuni
moja ya Florida, Marekani imekuja na dhana ya kujenga meli ‘Freedom
Ship’, itakayokuwa na uwezo wa kuwa na kila kitu cha kuifanya iwe jiji
linaloelea kwenye maji.
Wabunifu wa dhana ya meli hiyo wametoa picha za computer za kile wanachoamini meli hiyo itakavyokuwa pindi itakapokamilika.
Roger
M Gooch, mkurugenzi na makamu wa Rais wa kampuni ya Freedom Ship
International ya Florida, Marekani, ambao ndio wenye mradi huo, amesema
hiyo itakuwa ndio meli kubwa kuwahi kujengwa, na jiji la kwanza
linaloelea kwenye maji. ‘The Freedom Ship will be the largest vessel
ever built, and the first ever floating city.’
Uwanja wa ndege utakaokuwa juu ya meli itakayowezesha ndege kuruka na kutua hata wakati meli inatembea
Gooch,
Amesema kampuni yake inajaribu kukusanya kiasi cha £6 billion
zinazohitajika kuifanya ndoto hiyo iwe kweli, ambayo mpango wake
umekuwepo kwa miaka mingi.
“But
in the last six months we’ve been getting more interest in the project
and we are hopeful we will raise the $1billion (£600million) to begin
construction.’ The ship would spend 70 per cent of its time anchored off
major cities and the rest sailing between countries” Aliongeza.
Freedom Ship, itakuwa na huduma zote za jiji kama Shopping center, shule, hospitali, uwanja wa ndege, casino, parks nk.
Meli
hiyo inayotegemewa kuwa na ghorofa 25, itakuwa na uwezo wa kuwapa
makazi ya kudumu watu 50,000, lakini itakuwa na nafasi ya ziada ya
kupokea wageni wengine 30,000, makazi 20,000 ya wafanyakazi wa meli, na
mengine 10,000 kwaajili ya wageni wa usiku mmoja.
Hii ndio njia inayotarajiwa kutumiwa na meli hiyo kuizunguka dunia
Meli
hiyo inatazamiwa kuwa inazunguka dunia nzima nchi moja hadi nyingine,
bara moja hadi linge na itafika hadi Afrika, na haitakuwa ikikaa sehemu
moja kwa muda mrefu.
Itakuwa
na makazi ya watu 50,000 pamoja na makazi ya wageni 30,000 na makazi
20,000 ya wafanyakazi wa meli, na mengine 10,000 kwaajili ya wageni wa
usiku mmoja.
Meli
hiyo itakuwa na huduma zote za muhimu zinazopatikana katika majiji
mbalimbali zikiwemo hospitali, shule, maduka, parks, casino, aquarium,
kiwanja cha ndege chenye njia ya kuruka na kutua ndege ndogo zenye uwezo
wa kubeba watu 40, kitakachokuwa juu kabisa kwenye paa la meli hiyo.
Meli hiyo itakuwa ikitumia umeme wa solar pamoja na wave energy.
Itakapokamilika,
jiji linaloelea litakuwa na upana wa 750ft, urefu wa kwenda juu350 ft,
pamoja na urefu wa 4,500 ikiwa ni mara nne ya Queen Mary II Cruise ship
iliyokuwa na urefu wa 1,132ft.

Wageni na wenyeji wanauwezo wa kuondoka na kuingia kwenye jiji hilo la majini kwa ndege au boti

Meli
hii inatarajiwa kugharimu dola bilioni 10 mpaka kukamilika kwake, na
itakuwa na uzito wa tani milioni 2.5, lakini kwa sasa bado ni dhana
(concept) TOA MAONI YAKO APO CHINI








No comments:
Post a Comment