Dudubaya anajulikana kama mmoja wa Wasanii wa siku nyingi
bongoflevani ambae pamoja na headlines zake binafsi huwa anasikika mara
chache akizungumzia au kutoa ushauri kwa ishu kadhaa za Wasanii wenzake.
Baada ya kusikia yanayoendelea kati ya mastaa wa bongofleva Diamond
na Ally Kiba kwamba wako kwenye beef, Dudubaya alikutana na AyoTV Dar es
salaam na kuyasema yafuatayo >> ‘Wasanii wa Tanzania tuna wapambe
na sio marafiki kwa sababu mpambe unaweza kuwa umelewa yeye ndio
anakoleza ugomvi lakini rafiki ni yule anaekuonya au kukushauri’
Ali Kiba alifanya ngoma na R.Kelly nikafurahia na nikapenda kinoma
kupiga salute kwa mdogo wangu anakwenda next level, Diamond kaja kufanya
vizuri na ninafurahia… muziki huu unakosa nguvu kwa sababu ya roho
mbaya, wivu na chuki na kutokuwa makini na wanaotuzunguka, anakwenda kwa
Diamond anasema hivi kisha anakwenda kwa Ally Kiba anasema hivi’ –
Dudubaya
‘Ninachowashauri hawa wadogo zangu watulie chini wajitambue ni
Wasanii na usanii wao ni wa kutengeneza pesa, tena watengeneze hata Tour
ya Amani wazunguke nchi nzima.. wazunguke hata Afrika Mashariki na sio
hizi beef’
‘Siku moja nilikua na Dully Sykes na Christian Bella alafu watu
wakawa wanasema Diamond ooohhh sijui kashindaje tuzo saba, nikawaambia
hivi ukiwa na akili timamu wimbo kama ‘my number one’ kila kona
unayopita, video mpaka TV za kimataifa zinapiga alafu leo unaweza video
yako ya kijingajinga unategemea kuishinda ‘my number one’ …….Diamond
alistahili kushinda hizo tuzo saba, mimi sikuona cha ajabu’
Kwenye sentensi nyingine Dudubaya amesema ‘kuna gazeti moja
liliandika eti Diamond alihonga hela kuchukua hizo tuzo, ni vitu vya
kipumbavu kabisa… hujui kusoma lakini picha lazima uione, Ali Kiba na
Diamond kila mmoja ana mama yake, wakae chini kama binadamu wajitambue,
waachane na mambo ya watoto wa hapa mjini hawa ni wapambe tu mwisho wa
siku hawana msaada’
Tuesday, 29 July 2014
New
Yajue Maneno 120 ya Dudubaya baada ya kusikia kuhusu Diamond na Ali Kiba
About Cow Boy Bishoo Tz
SoraTemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of SoraTemplates is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment