NMB
leo imefungua tawi jipya katika mji maarufu wa Kibaigwa –Dodoma. Tawi
hilo litakuwa na huduma zote za kibenki kama yalivyo matawi mengine ya
NMB nchini kote.
Tawi la Kibaigwa limefunguliwa na Naibu spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni mbunge wa Kongwa, Mh Job Ndugai.
Kufunguliwa
kwa tawi la Kibaigwa kunafuatia mahitaji ya muda mrefu ya wateja wa NMB
wa eneo hilo wa kupata tawi lenye nafasi ya kutosha .Aidha eneo hili
ni karibu zaidi na wafanyabiashara wengi ambao ni wateja wakubwa wa NMB
na wananchi kwa ujumla .
Kwa
kutambua pia nia ya kuendelea kuchangia huduma mbali mbali za kijamii,
benki ya NMB inatoa shilingi Milioni 10 kwa ajili ya hospitali na shule
kama shukrani za Benki kwa wananchi wa Kibaigwa kwa kuendelea kwao
kuunga mkono maendeleo ya benki.
NMB ndiyo benki inayoongoza nchini kwa kuwa na matawi mengi kwani ina matawi zaidi ya 150, ATM Zaidi ya 500 nchi nzima pamoja na idadi ya wateja inayofikia Milioni mbili hazina ambayo hakuna benki yenye nayo
No comments:
Post a Comment