Pah One Warejea Tena na Wimbo Wa ‘Kizubaneta - COW BOY BISHOO

Breaking

Monday, 9 March 2015

Pah One Warejea Tena na Wimbo Wa ‘Kizubaneta

Baada ya Nahreel na Aika kujitoa na kuanzisha kundi lao, Navy Kenzo, kundi la Pah One limerejea tena likiwa na members wawili waliosaliaPah One wamesema ukimya wao ulitokana na shughuli zao za muziki ambazo zilizokuwa zikiendelea Congo, Ivory Coast na Afrika Kusini.
Wakiongea na E-News ya EATV, wawili hao wamedai kuwa wimbo mpya walioutoa unaitwa ‘Kizubaneta’. “Unajua hili jina maana yake ni kama kuzubaa na hii ni kazi ya tofauti na mashabiki wetu walivyotuzoea,” walisema.
“Unajua tulikuwa DRC katika show halafu tukaenda Ivory Coast ndio ambako tulitengeneza hii beat na kurekodi hii kazi yetu mpya na mwaka huu ndo tumeamua kurudi tena kwenye muziki.

No comments:

Post a Comment