Riyama na Keisha Kufanya Movie Kupinga Mauaji ya Albino!! - COW BOY BISHOO

Breaking

Monday, 9 March 2015

Riyama na Keisha Kufanya Movie Kupinga Mauaji ya Albino!!



Takribani kwa wiki mzima sasa Staa wa Bongo Movies, Riyama amekuwa akitoa ujumbe mzito akiitaka jamii kuacha na kupinga mauaji huku akisisitiza upendo kwa ndugu zetu mwenye ulemavu wa ngozi (Albinos) kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram.

Siku ya jana Riyama alibandika picha hiyo hapo juu akiwa na mwanamziki Keisha ambae ni mlemavu wa ngozi na kuandika kuwa wapo kazini, kitu ambacho mashabiki wake wengi walijiongeza kuwa Riyama na Keisha watakuwa Lokeshani wakitengeneza filamu ambayo bila shaka itakuwa ikihusiana na maswala ya kupinga mauaji ya ndungu zetu Albino.

Riyama aliandika

“Kazini Mungu bariki kazi ya mikono yetu...... ..Sambazaupendo tunawazaa sisi ni watoto wetu mamazetu baba zetu rafiki zetu Wao ni kama sisi tuwakumbatie tusiwabague ndugu zetu watanzania wenzetu ….”

Kama ni kweli watakuwa wanatengeneza filamu itakuwa imekaa poa sana. Kwa upande wa Keisha hii itakuwa sio mara yake ya kwanza kucheza filamu yenye maudhui ya kupinga mauaji ya Albino, kwani hapo nyuma alishawahi kucheza filamu ya aina hiyo.

No comments:

Post a Comment