Mjue IRENE LAVEDA, mshiriki wa BIG BROTHER AFRICA 2014 kutoka TANZANIA - COW BOY BISHOO

Breaking

Wednesday 8 October 2014

Mjue IRENE LAVEDA, mshiriki wa BIG BROTHER AFRICA 2014 kutoka TANZANIA

La Veda akiwa kazini.
MUZIKI: Kwa upande wa muziki, La Veda ni mkali sana wa kucheza na tarumbeta. Hii ni nadra sana kukutana na mwanamuziki ambaye anauwezo wa kupiga kifaa japo kimoja cha muziki.
Mrembo La Veda sio tu mkali wa kupuliza tarumbeta bali ameshatoa vibao mbalimbali kama UTANIMISS, SIMPLE LOVE, LET IT GO, na kibao kikali kinachotamba kwenye mitandao mbalimbali, kibao
ambacho kinaitangaza Tanzania katika sekta ya utalii kiitwacho TWENDE TUKATALII , Video ya wimbo huu inapatikana You tube.

La Veda katika pozi na baadhi ya mastaa.
Mrembo huyu ambaye ameshawahi kuingia 10 bora ya shindano la Miss Tanzania mwaka 2012, baada ya kutwaa taji la Miss Lindi 2012, anaingia rasmi leo tarehe 5 Oktoba 2014 kwenye shindano hilo lenye mashabiki
wengi duniani ambalo kuanzia saa 1 jioni litakua likirushwa live kupitia DSTV kwenye channel no. 198.
Irene Neema Vedastous aka Irene La Veda ni nani?
Irene La Veda, sio mrembo mpya kwenye jamii ya Watanzania kama wengi wanavyodhani, ni mrembo anayependa kujichanganya na watu mbalimbali. Hii hali imemuwezesha kufanya vitu mbalimbali na
vikubwa kwenye fani mbalimbali kama filamu, muziki, urembo, mitindo, nk.

Irene Neema Vedastous ‘La Veda’, Mshiriki wa Big Brother Hotshots kutoka Tanzania.
IRENE NEEMA VEDASTOUS ni msichana mrembo wa Kitanzania, mwenye umri wa miaka 23 anayeiwakilisha Tanzania katika shindano la BIG BROTHER 2014 ‘HOTSHOTS’ nchini Afrika Kusini.
La Veda (wa kwanza kulia) akiwa na baadhi ya washiriki wa Miss Tanzania 2012.
Mama Mzazi wa La Veda, Mecky Sebastian anasemaje kuhusu mwanaye kushiriki Big Brother Hotshots? msikie hapa;
“Naomba akina mama wenzangu, wasanii na Watanzania wote kwa ujumla mnisaidie katika kumuunga mkono La Veda ili aweze kuiletea heshima nchi yetu na yeyote popote alipo mwenye kuitakia mema
Tanzania na Afrika Mashariki tumpe ‘support’ ya kutosha ili aweze kuibuka mshindi. Nawatakia Watanzania kila la kheri kwenye shughuli zao za maendeleo”, alisema Mama Mzazi wa La Veda, Mecky Sebastian.

No comments:

Post a Comment